JE PUNYETO NI DHAMBI?

By MATHAYO DAUDI SUDAI
22nd November, 2021

Na je! Kuoa ni suluhisho la kuzuia tamaa kama biblia inavyosema katika
1Wakorintho 7:9?.

 Bwana Yesu alisema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake. Sentensi hiyo inaonyesha kuwa dhambi haianzii nje ya mwili bali inaanzia moyoni, hivyo zinaa pia inaanzia moyoni, ikishafanyika moyoni ndipo inatoka nje, kwahiyo chochote kinachofanyika mwilini ni matokeo ya kitu kilichofanyika tayari rohoni, hivyo uasherati, masturbation (punyeto), utazamaji wa pornography hayo yote ni matokeo ya uasherati ambao tayari yalishafanyika ndani ya moyo wa mtu.  

Ndio masturbation ni dhambi. Na suluhisho pekee la kuikwepa hiyo dhambi ni kumkabidhisha Bwana Yesu maisha yako ki-kweli kweli, na kudhamiria kuanza maisha mapya katika Kristo, na kuamua KUACHA!! Wengi wanatafuta kuombewa waache kutazama pornography au kufanya masturbation lakini hawajadhamiria kuamua kuacha hivyo vitu,..wanasubiria miujiza ishuke wajikute wameacha na huku bado mioyo yao inaelekea kwenye zinaa…Nataka nikuambie ndugu yangu unayemtafuta Mungu,Hakuna maombi yoyote ya kuondoa hicho kitu ndani ya mtu, ili hivyo vitu viondoke ni kuamua kwanza kuchukua uamuzi wa kuacha hayo mambo ndipo Bwana anakuongezea UWEZO wa kushinda hayo mambo,. Kumbuka na Biblia inasema waasherati wote sehemu yao ni katika ziwa la moto.   Na pia kuhusu kuoa biblia imeweka wazi katika kitabu cha

1 Wakorintho7 :1

Biblia inasema
 “Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.2 Lakini kwa sababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe”.

Ukisoma kwa makini huo mstari wa 2 anasema kwasababu ya ZINAA kila mtu mwanamume awe na mke wake mwenyewe…sio kwasababu ya KUEPUKA TAMAA…bali kwasababu ya ZINAA…na zinaa maana yake ni kufanya mapenzi nje ya ndoa au kabla ya ndoa, Hii ikiwa na maana kuwa, kuwa na mke hakumzuii mtu kulipuka tamaa…kama tabia ya mtu ni kutamani! Hiyo tabia hataiacha hata akioa au akiolewa..pengine ataepuka zinaa tu baada ya kuoa/kuolewa kwasababu atakuwa na mke/mume wake ndani!…. Lakini tama ya kutazama wanawake wengine itakuwa palepale kama atakuwa hajabadilishwa.  

Kwahiyo suluhisho pekee la kuzuia tamaa kwa aliyeoa au asiyeoa, ni kumkabidhi Kristo maisha kwanza, na kukusudia kuacha dhambi, (kumbuka Mungu hawezi kumsaidia mtu ambaye hajakusudia kwa dhati kuacha kile kitu kibaya anachokifanya)..mtu akishakusudia kuacha kwa vitendo tabia ya kutamani, kujitenga na vichochezi vyote vya uasherati, muvi zenye vimelea vya ngono ndani yake, pornography, matusi, maneno ya mizaha yasiyokuwa na maana, ndipo Roho Mtakatifu anakuja juu yake na kumsaidia na hivyo anajikuta vile vitu havimsumbui tena maishani mwake. Tofauti na yule anayetamani tu kuacha lakini haonyeshi jitihada yoyote ya kutaka hivyo vitu viondoke ndani yake.  kutazama picha za ngono mara nyingi humpelekea mwanaume afanye punyeto jambo ambalo ni baya sana mbele za mwenyezi mungu.

Ubarikiwe!

Tags:

This site was designed with Websites.co.in - Website Builder

WhatsApp Google Map

Safety and Abuse Reporting

Thanks for being awesome!

We appreciate you contacting us. Our support will get back in touch with you soon!

Have a great day!

Are you sure you want to report abuse against this website?

Please note that your query will be processed only if we find it relevant. Rest all requests will be ignored. If you need help with the website, please login to your dashboard and connect to support